Wadau watakiwa kushirikiana na Serikali katika
kutatua changamoto za kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii
yetu.
Akifungua kikao cha wadau
wa watoto na wanawake wa mkoa wa Arusha,mwenyekiti wa kikao hicho Richard
Kwitega, amesema bado jamii inatakiwa kupata elimu zaidi juu ya ukatili huu.
Amesema
kati ya mwaka 2017/2018 jumla ya watu 1,437 walifanyiwa ukatili wa kijinsia katika
Mkoa wetu wa Arusha, ambapo wahanga wakubwa ni wanawake na watoto na hawa ni
wale waliofika maeneo ya huduma kama vile polisi, Vituo vya Afya na Ustawi wa
jamii.
Kwitega
amesema kuna uwezekano mkubwa idadi hii ikaongezeka kwani si kila mtu
anaetendewa ukatili huu wa kijinsia anafika kutoa taarifa katika vituo husika,
wapo wanaoficha kwa kuogopa aibu katika jamii zao.
Aidha,amesema kuna madhara makubwa sana yanayotokana na
ukatili huo,ikiwemo kushindwa kujishughulisha na shughuli za kiuchumi na hivyo
kupelekea kushuka kwa pato ghafi la Taifa.
Akitoa shukrani kwa kuwakutanisha wadau na serikali
Mkurugenzi wa Railway Children Afrika
Musa Mgata, amesema kukutana kwao kumewapa nguvu zaidi ya kuendelea
kushirikiana na serikali kwa karibu zaidi ili kutokomeza ukatili wa kinjinsia
kwa wanawake na watoto.
Kikao cha wadau wa watoto na wanawake kwa mkoa wa Arusha
kimefanyika kwa lengo la kupitia Mpango Kazi wa Taifa wa
Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) na kuona ni kwa jinsi
gani wadau wanaweza kuisaidia Serikali kwa kutambua majukumu yao.